NIGERIA-MAJANGA YA ASILI

Mafuriko yaua watu wengi Nigeria

Wanawake wakipita katika maji ya yaliyosababishwa na mafuriko katika kambi ya Bakassi, Borno, Nigeria, Julai 18, 2017.
Wanawake wakipita katika maji ya yaliyosababishwa na mafuriko katika kambi ya Bakassi, Borno, Nigeria, Julai 18, 2017. REUTERS

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yameua watu zaidi ya 49, na wengine 20 bado hawajulikani waliko kwenye mpaka wa Nigeria na Niger, idara ya huduma za dharura nchini Nigeria imesema.

Matangazo ya kibiashara

Vijiji vitano katika wilaya ya Jibia vimekumbwa na mafuriko wakati mto ulipofurika maji na kuenea katika badhi ya maeneo ya vijiji hivyo usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu baada ya mvua kubwa kunyesha, mkurugenzi wa idara ya huduma ya DharuraAminu Waziri katika Jimbo la Katsina, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Tumepata miili 49 (kutoka vijiji vitano) na bado tunatafuta wengine 20," amesema.

Watu ishirini na wanne miongoni mwao walipelekwa hadi katika vijiji vya Mada Rumfa na Kantumi katika nchi jirani ya Niger.

"Baadhi ya waathirika waliondolewa chini ya vifusi vya nyumba zao zilizoanguka," Bw Waziri ameongeza.

Zaidi ya watu 2,000 walilazimika kutoroka makazi yao kufuatia mafuriko hayo na kukimbilia katika Shule ya Msingi ya Jibia, na wengine waliojeruhiwa 27 wamelazwa hospitali ya jimbo hilo.

Mafuriko hua yanatokea mara kwa mara katika sehemu nyingi znchini Nigeria wakati wa msimu wa mvua, ambao huanza Mei hadi Septemba.