UFARANSA-NIGER-USHIRIKIANo-USALAMA

Waziri wa majeshi wa Ufaransa ziarani Niger kuunga mkono kikosi cha G5 Sahel

Waziri wa Majeshi wa Ufaransa, Florence Parly, kulia, wakati wa mazungumzo na rais wa Niger Mahamadou Issoufou (wa pili kutoka upande wa kulia) huko Niamey, Niger, 4 Juni 2018.
Waziri wa Majeshi wa Ufaransa, Florence Parly, kulia, wakati wa mazungumzo na rais wa Niger Mahamadou Issoufou (wa pili kutoka upande wa kulia) huko Niamey, Niger, 4 Juni 2018. Twitter/ Florence Parly

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly ametembelea nchini Niger, kuunga mkono operesheni za jeshi la pamoja na G5 Sahel katika mapambano dhidi ya ugaidi katika ukanda wa Sahel.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa majeshi wa Ufaransa aliwasili nchini Niger siku ya Alhamisi kujadili kuhusu kikosi cha G5 Sahel na mwenzake wa Niger, Kalla Moutari na rais Mahamadou Issoufou.

Mkutano huu ni kuhusu "kuimarisha utaratibu wa kazi kwa kikosi hiki cha pamoja cha G5 Sahel", kulingana na mwelekeo uliofanywa katika mkutano wa Umoja wa Afrika huko Nouakchott mapema Julai, chanzo cha wizara ya majeshi ya Ufaransa kimesema.

Hii ni ziara ya saba ya Florence Parly katika ukanda huo. Niger sasa ni mwenyekiti wa G5 Sahel, kundi la nchi tano (Mali, Niger, Burkina Faso, Chad, Mauritania) ambalo liliunda kikosi cha pamoja cha jeshi kwa kupambana dhidi ya makundi ya kijihadi yanayopatikana katika eneo hilo.

Parly ametembelea kambi ya jeshi nchini humo lakini pia kuwatembelea wanajeshi wa Ufaransa baada ya kukutana na rais wa Niger Mahamadou Issoufou. Waziri huyo amesisitiza kuwa Ufaransa itaendelea kuunga mkono operesheni hiyo ambayo imefanikisha kuuawa kwa magaidi zaidi ya 120 kuanzia mwaka huu.