CHAD-USALAMA

Serikali ya chad yaishtumu Amnesty International "kudhoofisha jitihada" zake

Rais wa Chad Idriss Deby.
Rais wa Chad Idriss Deby. REUTERS/Alain Jocard/Pool

Serikali ya Chad imelishtumu shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty Internationa kwamba linalenga kudhoofisha jitihada zake. Serikali ya Chad imesema ripoti ya Amnesty International ya mwezi huu wa Julai inalenga kuipaka matope.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo ya Amnesty International inashtumu serikali kwamba imekua ikiendesha ukandamizaji kupitia vyombo vyake maalumu dhidi ya wapinzani na wale wanaoikosoa serikali ya nchi hiyo.

Ripoti hiyo yenye kichwa cha mhabari "kupungua kwa bajeti, ukandamizaji kwa kiwango cha juu" ya Amnesty International ina "habari zinazoegemea upande mmoja na imejaa madai ya uchochezi kama kudhoofisha juhudi za serikali ya Chad katika kuboresha utawala," kulingana na taarifa ya serikali iliyotolewa siku ya Jumapili.

"Chad imefanya maendeleo makubwa, hasa katika sekta ya afya, elimu na miundombinu," na wakati huo huo inakabiliwa na "makundi ya kigaidi" kwenye mipaka yake, taarifa hiyo imeongeza.

"Madai ya Amnesty International hayana msingi wowote ispokua kuchafua serikali kwa lengo la kutaka inyimwe msaada kutoa wafadhali wake,"serikali ya Chad imesema.

Ripoti ya Amnesty ilibainisha kupwakati ambapo visa vya ukandamizaji vimeongezeka. Kati ya mwaka 2013 na 2017, bajeti ya afya, kwa mfano, ilipungua kwa kiwango cha asilimia hamsini, na hivyo kusababisha uhaba wa dawa.