CHAD-USALAMA

Watu kadhaa wauawa na wengine watekwa katika shambulizi la Boko Haram Chad

Ziwa Tchad Julai 16, 2016 katika jimbo la Bol, mji mkuu wa mkoa wa Ziwa.
Ziwa Tchad Julai 16, 2016 katika jimbo la Bol, mji mkuu wa mkoa wa Ziwa. SIA KAMBOU / AFP

Habari inayoendelea kugongwa vichwa vya habari nchini Chad ni ya mauaji ya watu kadhaa nchini Chad wakati wapiganaji wa Boko Haram waliposhambulia kijiji kimoja karibu na Dabua kwenye mpaka kati ya Chad na Niger.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea siku ya Alhamisi jioni Julai 19. Watu wengi waliuawa na wengi kadhaa walitekwa nyara kaskazini mwa Ziwa Chad, upande wa Chad na sio mbali na Niger, wakati wa shambulio la kundi la hilo lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda. Makumi ya wanavijiji waliuawa na wanawake kadhaa walitekwa nyara.

Watu wengi waliuawa kwa kisu. "Walichinjwa," amethibitisha mkuu wa mkoa wa ziwa Chad, ambaye alikwenda kwenye eneo la tukio.

Wanawake zaidi ya ishirini pia "walitekwa nyara na washambuliaji ambao walikimbilia upande mwingine wa mpaka," chanzo cha kijeshi kimesema, huku kikibaini kwamba operesheni imezinduliwa ili kuwapata waathirika.

Mamlaka ya ziwa imewashtumu wakaazi wa kijiji hicho hasa wakulima kwa kutokuwa makini kwa kuendesha kazi zao katika maeneo yasio salama wakati wa majira ya baridi.

Shambulizi hili ni la kwanza tangu kuanza kwa majira ya joto. Jambo la mwisho lilikuwa Mei 6, wakati waasi walivamia kituo cha jeshi la Chad, na kuua askari sita na kujeruhi wengine watatu.