DRC-BEMBA-SIASA-USALAMA

MLC: Jean-Pierre Bemba atarudi Kinshasa Agosti 1

Mfuasi wa Jean-Pierre Bemba akiomba mbele ya picha ya aliyekuwa makamu wa rais wa DRC kwenye makao makuu ya chama cha MLC huko Kinshasa Juni 8, 2018.
Mfuasi wa Jean-Pierre Bemba akiomba mbele ya picha ya aliyekuwa makamu wa rais wa DRC kwenye makao makuu ya chama cha MLC huko Kinshasa Juni 8, 2018. © JOHN WESSELS / AFP

Chama cha MLC kimetangaza kwamba kiongozi wa chama hicho Jean-Pierre Bemba atarejea nchini DRC Agosti 1. Makamu wa zamani wa rais, pia seneta, aliteuliwa na chama chake kuwania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika nchini DRC Desemba 23.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ilimuachiliwa huru mnamo mwezi Juni baada ya kukata rufaa.

"Chama cha MLC, kinayo furaha kubwa ya kuwafahamisheni kwamba baada ya miaka kumi ya kutokuwepo nchini, Seneta Jean-Pierre Bemba Gombo atarejea nchini Jumatano, Agosti 1, " chama cha MLCkimeandika katika taarifa yake.

Chama cha MLC kimewatolea wito wananchi wa DRC, hususan wakaazi wa mji wa Kinshasa, kuja kumpokea kwa shangwe na vigelegele, kwa amani na furaha," Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu Eve Bazaiba.

Bemba, mwenye umri wa miaka 55, ambaye kwa sasayuko nchini Ubelgiji, aliachiliwa huru kwa uamuzi wa majaji wa ICC mnamo mwezi Juni. Alihukumiwa mnamo mwaka 2016 hadi kifungo cha miaka 18 kwa mauaji yaliyofanywa na wanamgambo wake nchini Jamhururi ya Afrika ya Kati mapema mwaka 2000. Mapema mwezi Julai, mwendesha mashitaka wa ICC aliomba kuongezwa miaka mitano jela katika kesi nyingne yinayohusiana na kuhonga mashahidi. Wanasheria wake mashitaka kufutiliwa mbali hayo dhidi yake.