DRC-KATUMBI-HAKI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais DRC: Moise Katumbi kurudi kabla ya Agosti 8

Watu walio karibu na Moise Katumbi, mshirika wa zamani wa karibu wa Joseph Kabila wametangaza kwamba mwanasiasa huyo aliyekimbilia uhamishoni, atarejea nchini kabla ya tarehe 8 Agosti, 2018.

Moise Katumbi atarudi DRC kabla ya Agosti 8, ndani ya muda uliowekwa na kalenda ya uchaguzi, msemaji wake ametangaza.
Moise Katumbi atarudi DRC kabla ya Agosti 8, ndani ya muda uliowekwa na kalenda ya uchaguzi, msemaji wake ametangaza. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa wanasheria wake, wanasema hakuna sababu inayomzuia mteja wao kurejea nchini DRC.

Mashtaka mawili dhidi ya Moise Katumbi yamesitishwa. Moja ya mashitaka hayo ni ni uasi, na kesi hiyo itasikjilizwa upya mnamo mwezi Oktoba, kesi nyingine inayomkabili ni ile ya upokonyaji wa mali za watu binafsi, kesi ambayo itasikilizwa katika Mahakama ya Rufaa na kuamuliwa ten upya.

Kuhusu mashtaka kwamba Moise Katumbi ni raia wa Italia,mashitaka yaliyotolewa na serikali ya DRC, msemaji wa Moïse Katumbi, Olivier Kamitatu, ameeleza kuwa vyombo vya sheria vya Italia tayari vimeamua kuhusu suala hilo: Moise Katumbi hajawahi kupewa uraia wa Italia.

"Jibu limekwishatolewa, Moise Katumbi hajawahi kusajiliwa katika ofisi ya serikali inayohusika na masuala ya uraia wa Italia na jibu hili lilikubaliwa na mahakamani na mwendesha mashitaka mkuu wa Milan.

Kesi zote dhidi ya Moise Katumbi nimeonekana kuwa zilitengenezwa na Moise Katumbi atarudi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndani ya muda uliowekwa na kalenda ya uchaguzi, kabla ya Agosti 8. Na kama atakamatwa atakapowasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - katika nchi yake - itakuwa ni haki isiyofaa na sio sheria.

Kama raia ana haki ya kulindwa na taasisi. Ikiwa atakamatwa, itakuwa uamuzi wa kibinafsi wa Joseph Kabila."