ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Upinzani walalama kuhusu wizi wa kura kabla ya uchaguzi Zimbabwe

Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare Julai 17, 2018.
Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare Julai 17, 2018. © AFP

Uchaguzi Mkuu wa Julai 30 nchini Zimbabwe, wa kwanza tangu Robert Mugabe kutimuliwa mnamo mwezi Novemba, "umeanza kufanyiwa udanganyifu," kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa ameshtumu.

Matangazo ya kibiashara

"Jeuri" ya tume ya uchaguzi "iliyoamua kutoweka wazi uchaguzi" na matumizi ya vyombo vya habari vya umma na mamlaka, yote hayo yanaonyesha kuwa uchaguzi huu "umeanza kugubikwa na udanganyifu", Bw Chamisa ameviambia vyombo vya habari huko Harare.

"Katika hatua hii, hatujui ni kadi ngapi za kupigia kura zilizochapishwa au wapi zilichapishwa (...) Kumekuwa na kukataa kwa utaratibu wa viwango vya kimataifa kwa kutoa taarifa ya vifaa vya uchaguzi", Nelson Chamisa amesema.

"Ni dhahiri kwamba ZEC (tume ya uchaguzi) meonyesha msimamo wake wapi inaegemea(...) ZEC imeamua kutosimami uchaguzi vilivyo na kubebelea bendera ya timu ya Emmerson Mnangagwa", rais, amekataa mgombea mkuu wa upinzani kwa uchaguzi wa rais.

Bw Chamisa pia amekosoa kitendo cha chama tawala cha Zanu-PF cha kutoa chakula kwa raia.

Hata hivyo, amefutilia mbali uwezekano wa kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi. "Hatuwezi kususia muhula wetu. Washindi hawapaswi kususia uchaguzi, ushindi hauepukiki," amesema.

"Mnangagwa anajua kuwa kushindwa ni lazima, tutakwenda kwa wingi kwenye uchaguzi na kumuangusha Emmerson Mnangagwa," amesema kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC).

Uchaguzi uliofanyika chini ya utawala wa Robert Mugabe mara kwa mara uligubikwa na udanganyifu na unyanyasaji. Mrithi wake, Emmerson Mnangagwa, makamu wake wa zaman, aliahidi kuwa uchaguzi utakua huru na wa wazi.

Amealika kwa mara ya kwanza tangu miaka kumi na sita waangalizi kutoka nchi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Madola, ambao wamekubali kuwa watahudhuria uchaguzi huo.