Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-MNANGAGWA

Mugabe:Zimbabwe sio nchi ya kidemokrasia

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe Phill Magakoe / AFP

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameushutumu utawala wa sasa kuwa unairudisha nyuma demokrasia na kwamba unaongoza nchi pasipo kuzingatia sheria. Kiongozi huyo wa muda mrefu pia ameapa kutochagua wagombea wa chama tawala cha Zanu PF.

Matangazo ya kibiashara

Mugabe ametoa matamshi hayo, siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa taifa hilo la kusini mwa Afrika hapo kesho. Mkutano wake na wanahabari umepeperushwa hewani na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa.

"Zimbabwe imekuwa nchi isiyoheshimu demokrasia na utawala wa sheria, nazungumza katika siku hii niliyoisubiri kwa muda mrefu.  Tuwaache watu wachague wakiwa huru. Nina imani ED (Emmerson Mnangagwa) pia ametaka watu wachague kwa uhuru.

Amekishutumu chama cha Zanu PF kwa kuondolewa njama za kumwondoa madarakani.

Mugabe aling'olewa madarakani Novemba 2017 baada ya jeshi kuingilia kati na kuchukua hatamu ya uongozi huku likiendesha oparesheni ya kuwasaka  wanasiasa waliokuwa wakiunga mkono kundi la G40, lililokuwa mstari wa mbele kumpigia upatu mke, Grace kurithi madaraka ya urais.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.