DRC-BEMBA-SIASA-USALAMA

Vurugu zatokea baada ya Jean Pierre Bemba kuwasili Kinshasa

Ndege ya Makamu wa zamani wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean-Pierre Bemba, iliwasili saa 9:25 asubuhi saa za Kinshasa. Jean-Pierre Bemba amerejea nyumbani baada ya miaka kumi na mmoja akiwa kizuizini na nje ya nchi yake.

Kwa mara ya kwanza Jean-Pierre Bemba akiingia DRC baada ya miaka 11 akiwa nje ya nchi na kizuizini, Agosti 1, 2018.
Kwa mara ya kwanza Jean-Pierre Bemba akiingia DRC baada ya miaka 11 akiwa nje ya nchi na kizuizini, Agosti 1, 2018. RFI/Florence Morice
Matangazo ya kibiashara

Vurugu zilitokea muda mfupi baada ya Jean-Pierre Bemba kuondoka uwanja wa ndege. Makamu wa zamani wa rais alipelekwa haraka hadi makao makuu ya chama chake cha MLC.

Jean-Pierre Bemba aliteuliwa na chama chake kuwania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika nchini DRC Desemba 23.

Kurejea kwa Jean-Pierre Bemba kunaonekana kusisimua upya na kutikisa siasa za DRC. Tayari chama tawala, PPRD, kimetoa tamko kuwa Bemba hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais nchini humo kufuatia makosa na kifungo alichotumikia baada ya kitengo cha mwanzo cha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kumkuta na makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, kabla ya kuachiliwa huru katika kitengo cha rufaa cha mahakama hiyo.

Jean-Pierre Bemba amekua Ulaya kwa miaka 12 huku miaka 10 akiwa alitumikia kifungo kutokana na ukikukwaji wa haki za binaadamu ulifanywa na wapiganaji wake katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya kati.

Makamu wa rais wa zamani wa DRC alifutiwa mashtaka na ICC jambo lilomfanya aweze kurudi nyumbani DRC.