Je ni sahihi kwa vyama vya siasa barani Afrika kutumia maandamano kudai haki nyakati za uchaguzi?

Sauti 09:49
Wafuasi wa upinzani wakiandamana katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare, Agosti 1, 2018
Wafuasi wa upinzani wakiandamana katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare, Agosti 1, 2018 REUTERS/Siphiwe Sibeko

Wafuasi wa Chama kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe wameandamana kushinikiza tume ya uchaguzi kutangaza matokeo ya urais. Mara kadhaa barani Afrika tumeshuhudia katika chaguzi vyama vya siasa vikitumia maandamano na wakati mwingine fujo kudai haki. Je ni sahihi? Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji wetu ili kupata maoni yao.