DRC-ANGOLA-USHIRIKIANO

Joseph Kabila azuru Angola

Rais wa DRC Joseph Kabila amewasili Alhamisi wiki hii katika mji kuu wa Angola, Luanda, kwa ziara ya siku mbili kwa mwaliko wa mwenyeji wake wa Angola Joao Lourenço.

Rais wa DRC Joseph Kabila Kabange ziarani Angola, siku sita kabla ya muda wa mwido wa kuchukua fomu za kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23, 2018.
Rais wa DRC Joseph Kabila Kabange ziarani Angola, siku sita kabla ya muda wa mwido wa kuchukua fomu za kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23, 2018. Twitter/RDCongoDiplomatie
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo inakuja siku sita kabla ya muda wa mwisho wa kuchukua fomu za kuwania uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 23.

"Mheshimiwa rais Joseph #Kabila aliwasili leo asubuhi (Alhamisi)#Luanda kwa ziara ya kiserikali baina ya nchi mbili kwa mwaliko wa mwenzake wa Angola J. Lourenço," kulingana na ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Congo iliyoandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

Kwa ziara hii hili ya "kiserikali baina ya nchi mbili", rais Kabila anaongozana na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Usafiri, Vyombo vya Habari na Nishati, ujumbe huo umebaini.

Mwishoni mwa mwezi Mei, baada ya kukutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, rais Lourenço alimtolewa wito rais Kabila "kuheshimu" mikataba inayotaka kufanyika kwa uchaguzi nchini DRC Desemba 23 bila yeye kushiriki.

Wakati huo huo, viongozi hao wawili walitoa wito wa kufanyika uchaguzi mnamo Desemba 23 kulingana na kalenda ya Tume ya Uchaguzi ya DRC (CENI). Serikali ya DRC iliona wito huo kama kuingilia masuala ya ndani ya DRC.

Balozi wa Kongo mjini Luanda akinukuliwa na gazeti la Jornal De Angola, aliutilia mbali "hali ya kutokuelewana" kati ya nchi hizo mbili.