DRC-EBOLA-AFYA

Serikali ya DRC yatangaza maambukizi mapya ya Ebola

DRC yaendelea kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola.
DRC yaendelea kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola. AFP Photo/Junior D. Kannah

Miezi kadhaa baada ya ugonjwa wa Ebola kuripotiwa nchini DRC, serikali ya nchi hiyo imetangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo mapya, hasa katika mkoa wa Kivu kaskazini, mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya imetangaza kwamba maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola yamegundulika katika maeneo ya Beni, mashariki mwa nchi hio.

Wakaazi wa maeneo mengi ya mashariki mwa DRC wameingiliwa na wasiwasi, kufuatia tangazo hilo.

Maambukizi makubwa yameonekana katika eneo la Mangina ambapo ni kilomita 30 tu kutoka mji wa Beni.

Hivi karibuni serekali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Shirika la Afya Duniani (WHO) walitangaza mafanikio na mwisho wa janga hilo la Ebola katika jimbo la Ecuador, magharibi mwa nchi.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka wizara ya afya ya DRC, Wizara ya afya imetoa taarifa kwa shirika la afya duniani WHO kuwa, vipimo 4 kati ya 6, vimekutwa na virusi vya ugonjwa huo, na bado vipimo vingine vinaendelea.

WHO inasema kuwa, Ebola ni tishio kubwa nchini DRC, huku ikiitaka serikali ya DRC kuwa wa kweli katika kutoa taarifa za ugonjwa huo katika hali ya kufanikisha mapambano ya kutokomeza Ebola nchini DRC.

Tayari nchi jirani zinazochangia mpaka wa mashariki ya DRC katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kama vile Rwanda na Uganda zimenza kuwakaguwa watu wanaoingia na kutoka nchini DRC, hasa wafanyabiashara wanaotumia mpaka huo.