ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Mnangagwa ashinda uchaguzi wa urais Zimbabwe

Emmerson Mnangagwa, ambaye alimrithi mtangulizi wake na kiongozi wa kihistoria Robert Mugabe baada ya kutimuliwa madarakani mwezi Novemba, ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Jumatatu Julai 30 nchini Zimbabwe.

Rais Mteule wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.
Rais Mteule wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo upinzai umepinga matokeo hayo ya uchaguzi ukidai kwamba kulifanyika udanganyifu wa kati wa zoezi la kuhesabu kura.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) usiku wa kuamkia leo imetangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zimbabwe, baada ya uchaguzi mkuu kufanikiwa kufanyika salama Julai 30, 2018.

Emmerson Mnangagwa wa Zanu-PF ameshinda Urais wa Zimbabwe katika uchaguzi wa kwanza wa Urais, baada ya Robert Mugabe kuondoka madarakani, Mnangagwa ameshinda kwa kupata zaidi ya aslimia 50 ya kura zote dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa kutoka MDC.

ZEC wametangaza kuwa Emmerson anashinda kiti hicho kwa kupata ushindi wa asilimia 50.8 ya kura zote halali zilizopigwa wakati mpinzani wake wa karibu kutoka MDC Nelson Chamisa akipata asilimia 44.3 ya kura zote.

Rais wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC), Priscilla Chigumba, alitoa matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais.
Rais wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC), Priscilla Chigumba, alitoa matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais. REUTERS/Philimon Bulawayo

Mshirika wa karibu wa zamani wa Robert Mugabe, aliyetimuliwa madarakani mnamo mwezi Novemba, ameshinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi kwa asilimia 50.8 ya kura dhidi ya mpinzani Nelson Chamisa ambaye alipata 44.3 %, Tume ya Uchaguzi (ZEC) imetangaza usiku wa kuamkia leo Ijumaa.