DRC-SIASA-KATUMBI-BEMBA

Bemba asikitishwa na hatua ya serikali kumzuia Katumbi kuingia nchini

Mwanasiasa wa upinzani  Jean-Pierre Bemba akiwahotubia wanahabari siku ya Ijumaa Agosti 3 2018 jijini Kinshasa
Mwanasiasa wa upinzani Jean-Pierre Bemba akiwahotubia wanahabari siku ya Ijumaa Agosti 3 2018 jijini Kinshasa REUTERS/Kenny Katombe

Aliyekuwa Makamu wa rais nchini DRC Jean Pierre Bemba amesikitishwa na hatua ya serikali ya DRC kumzuia Kiongozi wa upinzani aliyekuwa uhamishoni Moise Katumbi kuingia nchini DRC.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Kinshasa Bemba ameitaka serikali kuhakikisha uchaguzi ujao unashirikisha wanasiasa wote.

Jitihada za Kiongozi wa upinzani nchini DRC aliyekuwa uhamishoni Moise Katumbi kuingia nchini DRC hiyo jana ziligonga mwamba baada ya kuzuiwa na serikali ya Drc kuvuka mpaka akitokea zambia.

Hiyo jana aliripotiwa kuingia katika eneo la kasumbalesa nchini DRC ambapo ni umbali wa kilomita 95 kutoka Lubumbashi.

Katumbi aliishi uhamishoni nchini Ubelgiji tangu may 2016 baada ya kujiondoa katika chama tawala chake raisi Joseph Kabila.

Moise Katumbi alitangaza kwamba atawasili Lubumbashi Agosti 3, lakini ndege yake binafsi ilinyimwa kiblai cha kutua kufuatia madai ya meya wa jiji la Lubumbashi, Ghislain Robert Lubaba Buluma kusema ndege hiyo imekataliwa kutua au kupaa katika anga ya DRC pamoja na mashitaka yanayoendelea kumkabili Moise Katumbi.