SOKA-CAMEROON

Clarence Seedorf atajwa kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Cameroon

Clarence Seedorf, ametangazw akuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Cameroon, Leo Agosti 4, 2018
Clarence Seedorf, ametangazw akuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Cameroon, Leo Agosti 4, 2018 Daily Express

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu za Real Madrid, AC Milan, Ajax na Inter Milan Clarence Seedorf amatangazwa kuwa Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Cameroon, Indomitable Lions.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Michezo ya Cameroon imethibitisha kuajiriwa kwa Seedorf. Kutangazwa kwa Seedorf kunamaliza uvumi ulioenea kuhusu nani atachukua kibarua cha kuifundisha Cameroon tangu ilipoondoka Hugo Broos ambaye Januari mwaka jana aliiwezesha Cameroon kushinda taji la Afrika nchini Gabon.

Seedorf aliywahi kuichezea Timu ya Taifa ya Uholanzi 'Orange' zaidi ya mechi 80 atasaidiwa na mchezaji wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Uhokanzi Patrick Kluivert.

Cameroon itakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la mataifa Afrika zitakazochezwa mwakani kutoka Juni 7 hadi 30.