ZAMBIA-AMANI-DEMOKRASIA

Katumbi aisifu Zambia kwa kuimarisha amani na demokrasia

Mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi
Mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi Getty Images

Kinara wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moise Katumbi Chapwe amewatraka wananchi wa Zambia kuungana na raia wao Edgar Lungu, aliyedai anapigania maendeleo ya watu wake.

Matangazo ya kibiashara

 

Katumbi, amenukuliwa na gazeti la Lusaka Times la Zambia akieleza kuwa Zambia ni taifa lililopiga hatua za maendeleo kwa kuwa viongozi wake wanazingatia amani na kuheshimu demokrasia na utawala wa sheria.

Amesema utawala wa sheria uliopo nchini Zambia ni funzo kwa mataifa mengine ya Afrika.

Aidha, kiongozi huyo ametoa mwito kwa upinzani nchini Zambia kuunga mkono juhudi za serikali na kuongeza kuwa ukosoaji ni sehemu ya demokrasia.

Mwaka jana kinara wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, aliwekwa kizuizini kwa makosa ya uhaini, lakini baadaye akatolewa gerezani baada ya mashaurino baina ya serikali ya Zambia na jumuiya ya kimataifa.

Katumbi aliyekuwa na nia ya kuingia nchini DRC, alizuia kuingia nchini humo na badala yake alisalia katika Mji wa Kitwe nchini Zambia.

Hata hivyo, ripoti zinasema mwanasiasa huyo kwa sasa anaelekea barani Ulaya baada ya jaribio la kuingia nchini kwake kukwama.