MALI-SIASA-USALAMA-HAKI

Mvutano wa kisiasa kuhusu uchaguzi waendelea Mali

Soumaïla Cissé (katikati), kiongozi wa upinzani, pamoja na wagombea wengine wa urais walioshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi katikamkutano na waandishi wa habari, huko Bamako, Agosti 6, 2018.
Soumaïla Cissé (katikati), kiongozi wa upinzani, pamoja na wagombea wengine wa urais walioshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi katikamkutano na waandishi wa habari, huko Bamako, Agosti 6, 2018. REUTERS/Luc Gnago

Wakati tume ya uchaguzi nchini Mali inatarajia kutangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita, Jumatano wiki hii, wanasiasa wa upinzani nchini humo wametangaza kwamba hawakubaliano na matokeo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamelalamikia matokeo hayo na kusema hawatayakubali, na tayari wameamua kupeleka mashtaka mahakamani.

Kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé, amefungua mashtaka 20 katika Mahakama ya Katiba dhidi ya majaji sita wa mahakama ambao amesema wanaipendelea serikali.

Uchaguzi wa duru ya pili umepangwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu nchini Mali.

Uchaguzi huu wa duru ya pili utawakutanisha wagombea wawili ambao ni rais anaye maliza muda wake Ibrahimu Boubacar Keita na kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé, ambao walitimiza kura zinazohitajika kwa kuwania duru ya pili ya uchaguzi.

Ni mara ya pili Ibrahim Boubacar Keita na Soumaïla Cissé wanapambana katika diuru ya pili ya uchaguzi wa urais. Wanasiasa hawa wawili wanafahamiana kwa muda mrefu na wanashiriki katika siasa kwa miaka mingi. Mambo mengi kuhusu wawili hawa yanafanana.

Hata hivyo uchaguzi huu wa mwaka 2018 utakuwa kwao ni mara ya pili wanapambana katika uchaguzi wa urais. Mnamo mwaka 2013, Soumaïla Cissé alishindwa dhidi ya mshindani wake Ibrahim Boubacar Keita ambaye alipata zaidi ya 70%.

Mshindi wa Uchaguzi huu anatarajiwa kuwa na kibarua kikubwa cha kuendelea kuhakikisha kuwa usalama unaendelea kuwepo nchini humo, hasa Kaskazini mwa nchi hiyo.