COTE D'IVOIRE-MARIDHIANO-HAKI

Ouattara atangaza msamaha kwa Simone Gbagbo na wafungwa wengine 800

Simone Gbagbo wakati kesi yake ikisikilizwa Juni 1, 2016.
Simone Gbagbo wakati kesi yake ikisikilizwa Juni 1, 2016. ISSOUF SANOGO / AFP

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara ametangaza msamaha kwa Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo , wakiwemo watu wengine 800 ambao wamekuwa wamefungwa jela miaka 20 utokana na mzozo wa kisiasa mwaka 2010.

Matangazo ya kibiashara

Simone ambaye mumwe, Laurent Gbagbo, anashikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini nchini Uholanzi, amepata msamahama huu kutokana na kile rais Outtara anasema ni harakati za kitaifa za kuhubiri msamaha na mshirikamano wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Simone, anayejulikana kwa jina maarufu kama 'mwanamke mkakamavu' alikua amehukumiwa miaka 20 jela kwa uvamizi wa mamlaka ya serikali dhidi ya jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 uliosababisha vifo vya watu elfu 3.

Vita hivyo vilimalizika baada ya mumewe, Laurent Gbagbo kukamatwa na Umoja wa Mataifa na jeshi la ufaransa kumuunga mkono rais wa hivi sasa Rais Alassane Ouattara.

Bwana Gbagbo anakabiliwa na mashtaka ya kivita na mahakama ya kimataifa ya ICC, lakini ameendelea kukana madai hayo.