NIGERIA-SIASA-USALAMA

Vikosi vya usalama vyazuia wabunge kufanya vikao Nigeria

Rais wa Baraza la Seneti Bukola Saraki.
Rais wa Baraza la Seneti Bukola Saraki. REUTERS/Paul Carsten

Vikosi vya usalama nchini Nigeria vimezuia kwa muda wabunge kufanya vikao vyao, ikiwa ni katika muendelezo wa mvutano kati ya serikali na bunge pamoja na baraza la Seneti. Hali hii inatokea ikiwa imesalia miezi sita tu kabla ya uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye saa moja asubuhi watu wenye silaha ambao walikua wamefunika nyuso zao huku wakivaa sare za polisi na maafisa wa idara ya taifa ya upelelezi (Department of State - DSS) walikua wamepiga kambimbele ya milango ya majengo ya taasisi hizo, wakizuia wabunge, wafanyakazi na waandishi wa habari kuondoka.

Wabunge hatimaye waliweza kuruhusiwa kuingia kwenye ofisi zao mapema mchana, baada ya kupinga hatua hii.

Hakuna sababu rasmi zilizotolewa, lakini wabunge kadhaa wa upinzani waliozuiliwa nje ya jengo la bunge wameshtumu ofisi ya rais kutaka kuanzisha utaratibu wa kumng'atua mamlakani rais wa baraza la Seneti, ambaye anatoa ushirikiano mzuri na wabunge wa upinzani, kwa mujibu wa wabunge hao.

"Tulmevamiwa na vikosi vya usalama. Wenzetu hawawezi kwenda kazini," Seneta Ben Murray-Bruce, mwanasiasa wa chama kikuu cha upinzani Peoples Democratic Party (PDP) amelaani mbele ya waandishi wa habari.

"Tumepata taarifa kwamba maseneta wa APC (chama tawala) wanajaribu kupindua uongozi. Ni kinyume na kidemokrasia.," Ameongeza.

Hivi kaibuni wabunge kadhaa wa chama tawala cha APC wamekiahama chama hicho na kujiunga na chama cha upinzani cha PDP.