ZIMBABWE-EU-MAREKANI-SIASA-USALAMA

EU na Marekani washtumu mwenendo wa maafisa wa usalama wa Zimbabwe

Baadhi ya watu waliokamatwa, baada ya polisi kuzingira makao makuu ya chama upinzani cha MDC, wakifikishwa katika mahakama ya mji mkuu Harare.
Baadhi ya watu waliokamatwa, baada ya polisi kuzingira makao makuu ya chama upinzani cha MDC, wakifikishwa katika mahakama ya mji mkuu Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo

Umoja wa Ulaya na Marekani zimelaani hatua inayochukuliwa na maafisa wa usalama kuwahangaisha na kuwakamata wafuasi wa wa chama kikuu cha upinzani MDC.

Matangazo ya kibiashara

Shutuma hizi zimekuja baada ya wafuasi 27 wa chama hicho waliokamatwa wiki iliyopita, wakati wakiandamana kupinga madai ya wizi wa kura kuachwa huru kwa dhamana.

Hivi karibuni polisi ya Zimbabwe ilizuia kufanyika mkutano wa upinzani na waandishi wa habari, mkutano ambao ungelifanywa na mgombea mkuu wa wapinzani na mgombea aliyeshindwa uchaguzi Nelson Chamisa.

Polisi wakiwa wamlivalia mavazi yao maalumu yakuzuia mashambulizi ya mawe na vifaa vingine waliingia katika hoteli moja, ambapo kiongozi wa upinzani angelifanya mkutano na waandishi wa habari, na kuwalazimu waandishi wa habari kuondoka mara moja.

Emmerson Mnangagwa, alishinda uchaguzi wa urais kwa 50.8 %, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, ushindi ambao mpinzani wake wa karibu Nelson Chamisa ameupinga na kudai aliibiwa kura.