MALI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Raia wa Mali waendelea kusubiri duru ya pili ya uchaguzi

Rais wa Mali anayemaliza muda wake Ibrahim Boubacar Keïta (kushoto) atapambana na kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé (kulia) katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Agosti 12, 2018.
Rais wa Mali anayemaliza muda wake Ibrahim Boubacar Keïta (kushoto) atapambana na kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé (kulia) katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Agosti 12, 2018. © STR, ISSOUF SANOGO / AFP

Wapinzani walioshindwa wakati wa uchaguzi wa duru ya kwanza ya kuwania urais nchini Mali, wamekataa kuwaunga mkono wagombea wawili wanaosalia watakaopambana katika duru ya pili siku ya Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa hao Aliou Boubacar Diallona Waziri Mkuu wa zamani Cheick Modibo Diarra, wamesema hawawezi kumuunga mkono yeyote katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, rais Ibrahim Keita ambaye atakuwa katika kinyang'anyiro cha Jumapili ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi sikiu ya Jumapili na kuhimiza amani.

Hata hivyo, mpinzani wake Soumaila Cisse, ameendelea kuonesha wasiwasi kuhusu iwapo uchaguzi wa Jumapili utakuwa huru na haki huku akisisitiza kuwa aliibiwa kura katika duru ya kwanza.