DRC-SIASA-USALAMA

Majina ya wagombea urais kutangazwa Septemba 19 DRC

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Corneille Nangaa.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Corneille Nangaa. JOHN WESSELS / AFP

Raia wa DRC wanasubiri majina ya wagombea watakaowania urais mwezi Desemba. Lakini bado mgawanyiko umeendelea kujitokeza upande wa upinzani ambao wanajaribu kutafuta mgomba mmoja pekee ambaye atapambana na mgombea wa chama tawala na washirika wake katika uchaguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Tayari Tume ya Uchaguzi CENI imesema watu 25 waliomba kuwania urais, kumriti rais Joseph Kabila ambaye hatawania tena.

Majina ya wagombea wa mwisho yatatangazwa tarehe 19 mwezi Septemba.

Mgombea wa chama tawala cha PPRD anatatrajiwa kuwa Waziri wa zamani wa Mambo Emmanuel Ramazani Shadary, huku ikisubiriwa kuona iwapo wapinzani wanaungana na kuwa na mgombea mmoja.