MALI-SIASA-USALAMA

Rais mtarajiwa asubiriwa na changamoto mbalimbali Mali

Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Mali atakua na kibarua cha kufutia ufumbuzi wa matatizo ya usalama na kiuchumi.
Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Mali atakua na kibarua cha kufutia ufumbuzi wa matatizo ya usalama na kiuchumi. © REUTERS/Luc Gnago

Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Mali uliofanyika Jumapili Agosti 12, anasubiriwa na kibarua kigumu cha kupambana na utovu wa usalama hasa Kaskazini mwa nchi hiyo kutoka kwa makundi ya kijihadi.

Matangazo ya kibiashara

Pia atakua na kibarua kigumu katika nyanja ya elimu au ukosefu wa ajira kwa vijana, bila kusahau migogoro ya kijamii, ambayo inaendelea kuongezeka nchini humo.

Uchagui wa Jumapili Agosti 12 ulitishia na matukio ya kigaidi.

Mkuu wa kituo cha kupigia kura aliuawa kwa kupigwa risasi vituo kadhaa vilichomwa moto, huku baadhi ya vituo vya kupigia kura vikiamua kufunga kabla ya muda uliopangwa.

Wagombea katimka uchaguzi huo walikua ni wawili pekee, Soumaïla Cissé na rais anayemaliza muda wake Ibrahim Boubacar Keïta.

Duru ya kwanza ya Uchaguzi huu ulifanyika mwezi uliopita na kukosekana kwa mshindi aliyepata asilimia 50 ya kura.

Rais Keita baada ya kupiga kura Jumapili asubuhi jijini Bamako, alisema ana uhakika wa kuibuka mshindi, huku Cisse akisema ana matumaini ya kuibuka mshindi lakini anahofia wizi wa kura.

Cisse amekwenda katika Uchaguzi huu wa marudiano bila ya kufanikiwa kuwaunganisha wanasiasa wengine wa upinzani kumuunga mkono katika uchaguzi huu, suala ambalo wachambuzi wanasema huenda likamsaidia rais Keita kushinda.