NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Wanajeshi wa Nigeria wakaidi amri ya kwenda vitani dhidi ya Boko Haram

Baadhi ya wanajeshi wa Nigeria wamegoma kwenda vitani kukabiliana na Boko Haram, baada ya kufyatua risasi angani kupinga amri ya kwenda mstari wa mbele kukabiliana na kundi hilo.

Jeshi la Nigeria limendelea kuimarisha ngome zake katika maeneo mbalimbali ya nchi hasaa huko Maiduguri.
Jeshi la Nigeria limendelea kuimarisha ngome zake katika maeneo mbalimbali ya nchi hasaa huko Maiduguri. AFP
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimethibitisha hali hiyo na kuripoti kwamba mgomo huo uliendelea kwa takribani saa nane.

Kwa mujibu wa mashahidi askari walikataa kupanda ndege ambayo ilikuwa iwahamishe kutoka Maiduguri kwenda katika mji wa Marte karibu na nchi jirani ya Niger katika vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.

Hatu hiyo ya wanajeshi hao iliwashangaza wengi baada ya kukaidi amri ya uongozi wa jeshi wa kwenda vitani kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram.

Kwa mujibu wa chanzo cha jeshi nchini humo ambacho hakikutaja jina lake, hali ya kutotii amri miongoni mwa wanajeshi imeendelea kwa miaka nane sasa.

Jeshi la Nigeria limekua likikabiliana na kundi la Boko Haramu kwa miaka kadhaa, huku raia wakiendelea kuwa na hofu kufuatia hali yao ya usalama.