DRC, SUDAN KUSINI-ANGOLA-SIASA-USALAMA

Mustakabali wa kisiasa wa DRC na Sudan Kusini kujadiliwa Angola

Viongozi kutoka mataifa ya Afrika ya Kati na Kusini wanakutana hii leo jijini Luanda nchini Angola kujadili masuala mbalimbali ikiwemo Mustakabali wa kisiasa wa DRC kuelekea uchaguzi mkuu wa desemba 23.

Luanda, mji mkuu wa Angola ambako viongozi kutoka mataifa ya Afrika ya Kati na Kusini wanakutana
Luanda, mji mkuu wa Angola ambako viongozi kutoka mataifa ya Afrika ya Kati na Kusini wanakutana STEPHANE DE SAKUTIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo pia watajadili hatima ya mkataba wa kugawana madaraka Uliosahiniwa hivi karibuni huko Sudan Kusini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Angolo amesema kwamba katika mkutano huo kutazungumzia  hali ya kisiasa katika  ukanda na mbinu za kutatua mizozo inayojitokeza.

Manuel Augusto amesema, viongozi hao watajadiliana hasa kuhusu hali ya kisiasa nchini DRC kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amealikwa katika mkutano huo utakaowaleta pamoja viongozi kutoka DRC, Congo Brazaville, Afrika Kusini, Rwanda, Uganda na Gabon.

Vile vile katika mkutano huo kutazungumziwa kuhusu ushirikiano  katika biashara na kuwavutia wawekezaji nchini Angola.

Mkutano huo utaongozwa na rais wa Angola Joao Lourenco.