Habari RFI-Ki

Upinzani DRC wajipanga kusimamisha mgombea mmoja wa urais

Sauti 10:06
Jean Pierre Bemba, mmoja wa wanasiasa wa upinzani waliochukua fomu ya kuwania urais wa DRC
Jean Pierre Bemba, mmoja wa wanasiasa wa upinzani waliochukua fomu ya kuwania urais wa DRC REUTERS/Kenny Katombe

Viongozi wa vyama vya upinzani nchini DRC wameanzisha mchakato wa kumpata mgombea mmoja atakayechuana na mgombea wa chama tawala cha PPRD Ramadhan Shadary katika uchaguzi mkuu wa Disemba 23. Ikiwa upinzani utafaulu kuwa na mgombea mmoja utapata mafanikio katika uchaguzi huo?Fredrick Nwaka amezungumza na wsikilizaji wetu ili kupata maoni yao.