ZAMBIA-UCHUMI

Upinzani walalama juu ya kodi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii Zambia

Upinzani nchini zambia unasem ahautokubaliana na hatu ya serikali ya utozwaji kodi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Upinzani nchini zambia unasem ahautokubaliana na hatu ya serikali ya utozwaji kodi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. ©Facebook

Upinzani nchini Zambia unashtumu hutua ya serikali ya kuanzisha utozwaji wa kodi ya kila siku kwa wale wanaotumia mitandao ya kijamii na kupiga simu.

Matangazo ya kibiashara

hama kikuu cha upinzani cha UPND kinasema hatua ya serikali ya kuwatoza watumiaji wa huduma hiyo Dola 0.03 kila siku, inaonesha kuwa serikali ya rais Edgar Lungu haina maono.

Hatua hii ya serikali imekuja wakati huu raia wa Zambia wakilazimika kulipia mtandao ili kuwasiliana kwa sauti.

Hata hivyo, serikali inasema utafiti wake umeonesha kuwa raia wengi wa nchi hiyo sawa na asilimia 80 hutumia WhatsApp, Skype na Viber kupiga simu na hatua hii itasaidia katika ukusanyaji wa mapato.