NIGERIA-VYOMBO VYA HABARI-HAKI

Mwandishi wa habari aliyekataa kufichua vyanzo vyake aachiliwa huru Nigeria

Mwandishi wa habari aliyekamatwa mapema wiki hii baada ya kuchapisha makala ya siri na kukataa kufichua vyanzo vyake ameachiliwa huru kwa dhamana, mwajiri wake amesema.

Samuel Ogundipe, mwandishi wa habari kwenye tovuti ya habari ya mtandaoni ya Premium Times
Samuel Ogundipe, mwandishi wa habari kwenye tovuti ya habari ya mtandaoni ya Premium Times Premium Times/Twitter
Matangazo ya kibiashara

Samuel Ogundipe, mwandishi wa habari kwenye tovuti ya habari ya mtandaoni ya Premium Times, alikamatwa na wenzake wawili Jumanne wiki huko Abuja, kuhusiana na madai ya Bunge kudhibitiwa kwa muda na maafisa wa usalama wiki iliyopita.

Wenzake wawili waliachiliwa tangu wakati huo. Bw Ogundipe alisalia kizuizini, akishtumiwa kuchapisha ripoti iliyosainiwa na mkuu wa polisi Ibrahim Idris na kupelekwa kwa Makamu wa Rais Yemi Osinbajo tarehe 7 Agosti. Ripoti hii ilieleza kuhusika katika operesheni hiyo Lawal Musa Daura, mkuu wa idara ya ujasusi ya Nigeria (DSS), ambaye alifukuzwa kazi na ofisi ya rais.

Bw Ogundipe alifikishwa mahakamani huko Abuja siku ya Jumatano, bila wanasheria wake kufahamishwa na anelifikishwa tena mahakamani Agosti 20.

Lakini kwa mujibu wa Premium Times, alifikishwa tena katika mahakama hiyo leo Ijumaa asubuhina kuachiliwa kwa dhamana. Mwanasheria wa Samuel Ogundipe aliomba mteja wake aachiliwe, ombi ambalo lilipokelewa vema na mahakama.

Mnamo tarehe 7 Agosti, maafisa wa usalama waliofunika nyuso zao lifunga kwa saa kadhaa barabara zinazoingia na kutoka kwenye jengo la Bunge, huku wabunge, wafanyakazi wasiokua wabunge na waandishi wa habari wakilazimika kusalia katika jengo hilo.