MADAGASCAR-SIASA

Rais wa Madagascar kuwania katika uchaguzi ujao

Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina.
Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina. REUTERS/Lintao Zhang

Rais wa Madagasar Hery Rajaonarimampianina ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa atawania kwa muhula wa pili mfululizo katika uchaguzi wa urais wa Novemba 7 na Desemba 19 kama kutakua na duru ya pili ya uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Hapa hapa, miaka mitano iliyopita nilikubaliana na nyinyi na leo, nakubaliana kwa mara nyingine na nyinyi", amesema mbele ya waandishi wa habari waliokusanyika kwa tukio hilo katika hoteli moja huko Antananarivo.

"Nina uhakika nitafanya zaidi kuliko niliyokufanyieni," amesema rais Rajaonarimampianina, mwenye umri wa miaka 59.

Atapambana na wapinzani wawili na marais wa zamani, Andry Rajoelina (2009-2014) na Marc Ravalomanana (2002-2009), ambao tayari wametangaza kuwa watawania katika uchaguzi huo wa urais.

Kwa sasa, faili kumi na tatu zimewasilishwa kwa Mahakama Kuu ya Katiba.

Andry Rajoelina lakini pia mawaziri wawili wa zamani, Jean Omer Beriziky na Jean Ravelonarivo, ni wagombea rasmi na Marc Ravalomanana anatarajia kwasilisha fomu yake katika siku zijazo. Muda wa mwisho wagombea kuwasilisha fomu zao ni Agosti 21.