NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Kumi na tisa wauawa katika shambulio kaskazini mashariki mwa Nigeria

Askari akitoa ulinzi kwa mamia ya watu waliotoroka makaazi yao kutokana na mashambulizi ya kundi la Boko Haram katika kambi ya wakimzi wa ndani ya Maiduguri, katika Jimbo la Borno.
Askari akitoa ulinzi kwa mamia ya watu waliotoroka makaazi yao kutokana na mashambulizi ya kundi la Boko Haram katika kambi ya wakimzi wa ndani ya Maiduguri, katika Jimbo la Borno. AFP/STRINGER

Watu kumi na tisa wameuawa katika shambulizi dhidi ya kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria, mashahidi wamesema. Mfanyakazi mmoja wa shirika la kibinadamu ambaye hakutaja jina lake amesema watu zaidi ya 63 waliuawa katika shambulio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, shambulizo hilo lilitokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili katika kijiji cha Mailari, katika jimbo la Borno.

Abatcha Umar, ambaye alinusurika shambulizi hilo, ameongeza kuwa hawezi kuthibitisha kuwa washambuliaji walikuwa wanamgambo wa kundi la Boko Haram au wapiganaji wa kundi la Islamic State katika eneo la Afrika Magharibi.

Ameongeza kuwa wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha walionekana wiki iliyopita katika kijiji jirani na kuwa tahadhari ilitolewa kwa askari waliokuwa wakipiga kambi katika mji jirani wa Gudumbali. Hakuna hatua iliyochukuliwa, amesema Bw Umar.

Mamia ya wakaazi w eneo hilo walilazimika kutoroka makaazi yao na kukimbilia katika kambi, amesema mfanyakazi wa sirika la kibinadamu.