DRC-AFRIKA KUSINI-USHIRIKIANO

DRC yakataa Thabo Mbeki kama mjumbe maalum wa Afrika Kusini

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, Julai 18, 2018 huko Johannesburg.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, Julai 18, 2018 huko Johannesburg. © GULSHAN KHAN / AFP

Afrika Kusini imemteua rais wa zamani wa nchi hiyo Thabo Mbeki kama mjumbe maalum wa nchi hiyo katika Kanda ya Maziwa Makuu. Lakini serikali ya Kinshasa imefutilia mbali hatua hiyo ya Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa Afrika Kusini inalenga kurejesha nafasi yake ya kusimamia amani, iko mbali kabisa kufaulu. Kauli hiyo ni ilijitokeza baada ya mkutano wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

"Tutashuhudia kurejea kwa Afrika Kusini katika Kanda ya Maziwa Makuu? Tangu kufika Cyril Ramaphosa kuingia madarakani, Afrika Kusini inalenga kurejesha ushawishi wake. Afrika Kusini inataka hasa kuwekeza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Maafisa kadhaa ambao hawakutaja majina yao wamesema. Lakini kama inavyothibitishwa na kura ya veto ya serikali ya Kinshasa, dhidi ya hatua hiyo ya uteuzi wa rais wa zamani wa Mbeki, Afrika kusini bado haijafaulu.

Thabo Mbeki anachukuliwa kama mmoja wa waasisi wa mchakato wa mpito nchini DRC, "rafiki wa Congo," anasema mchambuzi Stephanie Wolters, mkurugenzi wa kitengo cha "Kuzuia Migogoro" katika Taasisi ya Mafunzo ya Usalama Afrika nchini Afriika Kusini (ISS). "Kumkataa Thabo Mbeki ni kama kufunga milango yote," anasema. Mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa rais Kabila anathibitisha kuwa pendekezo hili limekataliwa. Lakini Barnaba Kikaya anahakikisha kuwa ni "mambo ambayo yamepitwa na wakati".

Utaeleza vipi kuwa baada ya mkutano wa SADC, wakati ambapo marais wa DRC na Afrika Kusini walikutana kwa siku tatu, ofisi ya rais wa Afrika Kusini inathibitishia vyombo viwili vya habari vya Afrika Kusini kwamba Bw Mbeki atakuwa mjumbe wake maalum mjini Kinshasa, kabla ya kutengua kauli hiyo siku ya Jumatatu asubuhi? Na kwamba msemaji wa serikali ya DRC alithibitisha uteuzi huu kwanza kabla ya kutengua kauli yake?

Ni kweli kwamba DRC ilikuwa imekataa wajumbe wengine maalum kama yule wa SADC, kwa hoja kwamba nchi haitawakubali. "Kwa kweli, ni aibu kwa Afrika Kusini kuona mjumbe wake anakataliwa hadharani," anasema mtaalam.

Itakumbukwa kwamba katika mkutano wa SADC, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alikuwa miongoni mwa marais ambao walimshawishi Joseph Kabila kuhutubia taifa kuwa anaachia ngazi.