ZIMBABWE-UCHAGUZI-HAKI

Kesi kuhusu uchaguzi yaanza kusikilizwa Zimbabwe

Siku moja baa makabiliano mabaya yaliyosababisha vifo, polisi ya Zimbabwe yazingira makao makuu ya chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) huko Harare tarehe 2 Agosti 2018.
Siku moja baa makabiliano mabaya yaliyosababisha vifo, polisi ya Zimbabwe yazingira makao makuu ya chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) huko Harare tarehe 2 Agosti 2018. REUTERS/Mike Hutchings

Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe inaanza kusikiliza leo, kesi ya chama kikuu cha upinzani MDC kupinga matokeo yaliyompa ushindi rais Emmerson Mnangangwa.

Matangazo ya kibiashara

Nelson Chamisa alikwenda Mahakamani baada ya kudai kuibiwa kura wakagti wa Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwezi Julai.

Nacho chama cha rais Mnaganagwa Zanu-PF kimekwenda mahakamani kutaka kesi hiyo kutupiliwa mbali.

Upinzani nchini humo unasema Tume ya Uchaguzi ilimsaidia Mnangangwa kupata ushindi, na kura za mgombea wake Nelson Chamisa ziliibiwa.

Wakili wa upinzani Thabani Mpofu, amesema tayari upinzani umeandaa ushahidi wa kutosha kuonesha namna kura zilivyoibiwa, na uko tayari kupambana na Tume ya Uchaguzi katika Mahakama hiyo ya Kikatiba.