DRC-AFYA-AEBOLA

DRC yajaribu kutokomeza ugonjwa hatari wa Ebola

Maafisa wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamevaa nguo zinazowakinga na maambukizi ya virusi vya Ebola wakati mafunzo ya kukabiliana dhidi Ebola karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini.
Maafisa wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamevaa nguo zinazowakinga na maambukizi ya virusi vya Ebola wakati mafunzo ya kukabiliana dhidi Ebola karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini. REUTERS/Samuel Mambo/File Photo

Wizara ya afya nchini DRC imekubali, kutumiwa kwa dawa nyingine nne kuona iwapo inaweza kuwasaidia watu walioambukizwa ugonjwa hatari wa Ebola Mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, maafisa wa afya walianza kutoa dawa inayofahamika kama mAb114 iliyotenegzwa nchini Marekani, kuona iwapo itawasaidia walioathiriwa.

Shirika la afya duniani WHO linasema watu 55 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu tangu kuzuka mnamo mwezi Agosti katika mji mdogo wa Mangina, kilomita thelathini magharibi mwa mji wa Beni.

Ugonjwa huo ukiwa unaambukizwa kwa kupitia kumgusa mgonjwa na kwa njia nyinginezo, kuripuka kwake katika mji mdogo wa Mangina, pamoja na mji wa Beni, kumezusha wasiwasi miongoni mwa wakazi wa mji wa Beni.

Ugonjwa huo uliozuka siku chache tu baada ya serikali ya DRC kutangaza mwisho wa ugonjwa wa Ebola katika nchi hii.

Tatizo kubwa katika eneo hili ni kuwa, watu wanao uzoefu wa kula nyama za pori, bila ya kujuwa ikiwa nyama hizo zinazouzwa mitaani ni za wanyama waliouawa na wawindaji, au walifariki porini kwa magonjwa.

Kupigwa marufuku uwindaji, uuzaji na ulaji wa nyama toka mbuga za wanyama na taasisi inayohusika na kuhifadhi wanyama wa porini ICCN, kunaonekana kutoheshimiwa na wakazi, wanaowinda, kuuza na kula nyama za pori.