ZIMBABWE-UCHAGUZI-HAKI

Uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya uchaguzi kutolewa Ijumaa Zimbabwe

Maafisa wa polisi wa Zimbabwe mbele ya mahakama tarehe 22 Agosti 2018, muda mfupi kabla ya Mahakama ya Katiba kuanza kusikiliza hoja za upinzani, ambao unapinga matokeo ya uchaguzi.
Maafisa wa polisi wa Zimbabwe mbele ya mahakama tarehe 22 Agosti 2018, muda mfupi kabla ya Mahakama ya Katiba kuanza kusikiliza hoja za upinzani, ambao unapinga matokeo ya uchaguzi. Jekesai NJIKIZANA / AFP

Siku ya Ijumaa, Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi rais Emmerson Mnangagwa, baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Julai.

Matangazo ya kibiashara

Mawakili wa kiongozi mkuu wa upinzani Nelson Chamisa wamekuwa wakieleza namna wizi wa kura ulivyofanyika, na kutaka Mahakama kutupilia mbali ushindi huo.

Mbele ya majaji tisa wa mahakama ya juu zaidi nchini Zimbabwe, wanasheria wa Movement for Democratic Change (MDC) kwa muda mrefu wametaja makosa ambayo, wanaona kuwa yalihusika kuvuruga uchaguzi wa Julai 30, uchaguzi wa kwanza tangu Robert Mugabe kutimuliwa madarakani miezi nane iliyopita.

Nacho chama cha rais Mnangangwa ZANU PF, kinataka kesi hiyo kutupiliwa mbali.

Bw Mnangagwa ambaye alipeperusha bendera ya chama cha Zanu-PF katika uchaguzi wa urais alishinda kwa 50.8% ya kura dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa, ambaye alipata 44.3% ya kura.

Mahakama inaweza kuthibitisha matokeo, kutoidhinisha na kupiga kura upya au kuagiza kurudiwa kuhesabu upya kwa sauti za kura.

Kukata rufaa kwa chama cha MDC tayari kumesababisha kuahirishwa kwa sherehe ya kutawazwa rais Mnangagwa, ambayo awali iliyopangwa kufanyika Agosti 12. Ikiwa Mahakama itathibitisha ushindi wake, sherehe itafanyika ndani ya saa arobaini na nane baada ya uamuzi wa Mahakama ya Katiba.