Habari RFI-Ki

DRC yasema haitaki msaada wenye masharti kuandaa Uchaguzi Mkuu

Imechapishwa:

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inasema, haitaki msaada wa masharti kutoka kwa Umoja wa Mataifa, ambao umesema, uko tayari kusaidia, kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba unakuwa huru na haki. Wakati uo huo, serikali ya DRC inasema, iko tayari kuandaa Uchaguzi huo bila ya msaada wowote kutoka nje. Je, serikali ya DRC kupitia tume ya Uchaguzi CENI, inaweza kuandaa Uchaguzi, utakaokuwa huru na haki peke yake ?

Rais wa DRC Joseph Kabila
Rais wa DRC Joseph Kabila REUTERS/Kenny Katombe