DRC-UN-HAKI

Kesi ya mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa yasikilizwa DRC

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa Zaida Catalan (picha ya 2009) na Michael Sharp waliuawa huko Kasai mwezi Machi 2017.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa Zaida Catalan (picha ya 2009) na Michael Sharp waliuawa huko Kasai mwezi Machi 2017. © BERTIL ERICSON, TIMO MUELLER / TT News Agency / AFP

Kesi ya watu wanaoshtumiwa kuhusika katika mauaji ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilifunguliwa bila kutarajia nchini DRC Jumatatu (Agosti 27). Jambo ambalo liliwashangaza wengi.

Matangazo ya kibiashara

RFI ilifanya uchunguzi kuhusu kesi hii na ilionyesha kuwa mauaji ya Michael Sharp, raia wa Marekani na Zaida Catalan, raia wa Sweden yaliandaliwa na kuwezeshwa na maafisa wa serikali, idara ya ujasusi ya DRC (ANR) na jeshi. Mmoja wa washtumiwa, Jose Tshibuabua alikamatwa kwa shinikizo la Umoja wa Mataifa, lakini hakuepo mahakamani Jumatatu wiki hii, wala hayupo kwenye orodha ya watuhumiwa waliorodheshwa na mahakama.

Hata hivyo alishtakiwa rasmi mnamo mwezi Desemba mwaka jana kwa kula njama katika mauaji ya wataalam hao. Kwa mujibu wa idara ya ujasusi ya DRC (ANR), wakati wa tukio, alikuwa mpashaji habari tu waidara hiyo. Lakini baada ya mauaji ya Michael Sharp na Zaida Catalan aliteuliwa kuwa kuwa afisa wa serikali.

José Tshibuabua wakati alipokamatwa alikuwa Mkurugenzi katika mamlaka ya uhamiaji. Idara ya ujasusi (ANR) ndio ilimkamata na idara hiyo inabaini kwamba kitendo alichokifanya alikitekeleza kwa nia yake mwenyewe.

José Tshibuabua hakuwapo kesi hiyo ilifunguliwa Jumatatu wiki hii, jambo ambalo liliwashangaza wengi.

Kwa upande mwingine, watuhumiwa wawili wapya walionyeshwa mahakamani. Watu hao wawili ambao walijitambulisha kama Vincent Manga, mkaazi wa Gombe, na Constantin Tshidime anayefahamika kwa jinala Bula Bula, mkuu wa jadi wa kundi la Moyo Musuila. Sio mbali na makaazi yao ambapo wataalam walikutwa waliuawa. Serikali inadai kuwa watu hao ni wahusika wakuu katika mauaji ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa.

Kesi hiyo ilisikilishwa muda wa saa 4, ambapo Bula Bula alimshtumu mtuhumiwa mwenzake Vincent Manga kwamba kama kiongozi wa kundi la wanamgambo, alimfanyia vitisho vya kumuua na kumlazimisha kukubali watu wake katika eneo analoongoza.

Serikali inadai kuwa wanamgambo hao ndio waliwau wataalamu wa Umoja wa Mataifa. Vincent Manga alisema kuwa alipokea amri kutoka kwa Kananga. Vincent Manga anatarajia kujibu mahakama Alhamisi wiki hii. Jumatatu hii, alihakikishia mahakama kwamba hamjui Constantin Tshidime anayefahamika kwa jina la Bula Bula.