DRC-ICC-NTAGANDA-HAKI

Bosco Ntaganda ashtumiwa kuwapa madawa ya kulevya askari wa watoto

Kiongozi wa zamani wa kivita DRC Bosco Ntaganda wakati kesi yale ilianza kusikilizwa mbelea ya ICC, Hague, Septemba 2, 2015.
Kiongozi wa zamani wa kivita DRC Bosco Ntaganda wakati kesi yale ilianza kusikilizwa mbelea ya ICC, Hague, Septemba 2, 2015. REUTERS/Michael Kooren

Kiongozi wa zamani wa kivita nchini DRC Bosco Ntaganda ameshtumiwa kuwapa madawa ya kulevya na pombe askari watoto kabla ya kuwatuma kuua maadui zake huko Ituri, mashariki mwa DRC, wawakilishi wa waathirika wamesema Jumatano wiki hii mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Matangazo ya kibiashara

Waasi wa zamani "walihusika moja kwa moja katika kuajiri maelfu ya watoto" ambao baadaye "walitumiwa kushiriki, baada ya kupewa madawa ya kulevya na pombe" katika operesheni za "kuua, kubaka na kupora mali ya adui, "amesema mwakilishi wa waathirika 298, Sarah Pellet.

Jumanne wiki hii upande wa mashtaka ulionyesha orodha ya visa vya mauaji vilivyotekelezwa chini ya amri ya Ntaganda mnamo mwaka 2002 hadi 2003, wakati wa ufunguzi mbele ya ICC awamu ya mwisho ya kesi yake.

Ntaganda ambaye anafahamika kwa jina la "The Terminator" anakabiliwa na makosa 13 ya uhalifu wa kivita na matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambayo alikana mnamo Septemba 2015. Anashutumiwa kuwa ameamuru mauaji, uporaji na ubakaji uliofanywa na askari wake.

Maazimio ya mwisho yalifunguliwa Jumanne wiki hii karibu miaka mitatu baada ya kesi ya Ntaganda kuanza kusikilizwa ICC mjini Hague, ambapo kiongozi huyo wa zamani wa kivitaanazuiliwa.