ETHIOPIA-AJALI-USALAMA

Ethiopia: Watu 18 wapoteza maisha katika ajali ya helikopta ya kijeshi

Watu kumi na nane wamepotza maishakatika ajali ya helikopta ya kijeshi iliyotokea leo Alhamisi Agosti 30 katika mkoa wa Oromo, kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, televisheni Fana BC imeripoti kwenye tovuti yake.

Askari 15 wa jeshi la Ethiopia wapoteza maisha katika ajali ya helikopta ya kijeshi, Oromo, kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Askari 15 wa jeshi la Ethiopia wapoteza maisha katika ajali ya helikopta ya kijeshi, Oromo, kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Watu wote waliokua ndani ya helikopta hiyo, wajeshi 15 na raia wa kawaida watatu, wamepoteza maisha katika ajali hiyo.

"Helikopta hiyo, ambayo ilikuwa ya Wizara ya Ulinzi, ilianguka wakati ilikua ikijaribu kupaa angani kutoka Dire Dawa, kaskazini-magharibi mwa Ethiopia, kwenda Bishoftu (kilomita 40 kusini-mashariki mwa Addis Ababa) na ilikua na watu 18 ", televisheni Fana BC imeripoti, bila hata hivyo kutoa taarifa yoyote kuhusu sababu za ajali ya helikopta hiyo.

Mnamo mwaka 2013, ndege ya mizigo ya kijeshi ya Ethiopia ilianguka wakati ilipokua ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu nchini Somalia, na kuua watu wanne kati ya sita waliokuemo.