DRC

Msanii wa DRC na mkosoaji wa rais Kabila atoweka

Rais wa DRC Joseph Kabila.
Rais wa DRC Joseph Kabila. REUTERS/Kenny Katombe

Msanii mchanga wa muziki wa kufoka foka na mkosoaji wa rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, amepotea tangu Jumatano msemaji wake ameiambia AFP jana Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Msanii huyo Bob Elvis Masudi ametoweka tangu Juamatano wakati alipokuwa akienda nyumbani kwa mzalishaji wa muziki wake kwa maandalizi ya kutoa albamu yake mpya, msemaji wake Willy Kanyinda amesema.

Hata hivyo mkuu wa polisi jijini Kinshasa Sylvano Kasongo ameiambia AFP kuwa ameshangazwa na taarifa hizo kwa kuwa hakuna yeyote katika familia yake aliyetoa taarifa polisi kuhusu kupotea kwake.