MISRI

Rais Sisi aidhinisha sheria inayodhibiti matumizi ya mitandao

Rais wa Misri  Abdel Fattah Al Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi REUTERS

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amethibitisha sheria inayozipa mamlaka haki ya kufuatilia watuamiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo kama sehemu ya kuimarisha udhibiti wa mitandao, gazeti la serikali limearifu jana Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuidhinishwa na bunge mwezi Julai, Baraza Kuu la Sheria za Vyombo vya Habari litakuwa na uwezo wa kuwaweka chini ya usimamizi watumiaji wa mitandao wenye wafuasi zaidi ya 5,000 - kwenye mitandao ya kijamii, blog binafsi au tovuti.

Aidha baraza hilo litakuwa na mamlaka ya kusimamisha au kuzuia akaunti yoyote binafsi ambayo "inachapisha au kutangaza habari bandia au taarifa yoyote inayochochea ukiukaji wa sheria, vurugu au chuki.