ZIMBABWE-UN-KILIMO-UCHUMI

UN kutoa misaada ya chakula kwa Wazimbabwe zaidi ya milioni moja

Msaada wa chakula ukitolewa kwa wananchi wa Zimbabwe huko Mutawatawa, karibu kilomita 220 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Harare, Novemba 25, 2013.
Msaada wa chakula ukitolewa kwa wananchi wa Zimbabwe huko Mutawatawa, karibu kilomita 220 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Harare, Novemba 25, 2013. REUTERS / Philimon Bulawayo

Umoja wa Mataifa unajiandaa kutoa msaada wa dharura kwa raia zaidi ya milioni moja wa Zimbabwe ambao wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa kilimo unaosababishwa na ukame unaoendelea nchini.

Matangazo ya kibiashara

WFP inajiandaa kutoa huma ya haraka kwa watu 1,135,500 wakati wa msimu wa kilimo (Januari-Aprili) 2018-2019.

Eneo la Afrika kusini mashariki linakabiliwa na ukame unaoendelea kwa miaka kadhaa, na madhara yake yanazidi kuongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewaikiwa ni pamoja na vimbunga kama El Nino.

Zimbabwe imekumbwa na mdororo mkubwa wa kiuchumi na kifedha tangu mwanzoni mwa mwaka wa 2000, mgogoro uliosababishwa na sera ya kupokonya kwa nguvu mashamba ya wazungu, uamuzi ulichukuliwa na Rais Robert Mugabe.

Mrithi wake Emmerson Mnangagwa, aliyechaguliwa mwezi uliopita kwa muhula wa miaka mitano, aliahidi kuendeleza uchumi, ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi kwa wawekezaji kigeni.