AFRIKA-ASIA-ULAYA-UNHCR-WAHAMIAJI

UNHCR: Wahamiaji wengi wamepoteza maisha katika bahari ya Mediterania

Wahamiaji waliokolewa katika Bahari ya Mediterania na shirika la kihisani la  SOS Méditerranée, Juni 12, 2018.
Wahamiaji waliokolewa katika Bahari ya Mediterania na shirika la kihisani la SOS Méditerranée, Juni 12, 2018. Karpov / SOS Mediterranee/

Bahari ya Mediterania imesababisha "vifo vingi kuliko hapo awali" kwa wahamiaji katika miezi ya kwanza ya mwaka 2018. Watu zaidi ya 1,600 wamepoteza maisha tangu mwanzoni mwa mwaka, kulingana na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) iliyotolewa Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kati ya mwezi Januari na Julai 2018, "watu zaidi ya 1,600 walipoteza maisha au walitoweka wakijaribu kuingia Ulaya," UNHCR imesema katika taarifa yake.

"Wakati idadi ya watu wanaowasili Ulaya imeshuka (-41%), kiwango cha watu wanaopoteza maisha wakijaribu kuingia Ulaya kimeongezeka kwa haraka," inasema ripoti ya shirika hilo, yenye kichwa cha habari "Safari za Kutisha", ikisema kuwa kati ya Januari na Julai, "mmoja kati ya watu 18" aliyejaribu kuvuka bahari ya Mediterania alipoteza maisha au kutoweka baharini, wakati "ilikuwa mmoja kati ya watu 42 wakati huo huo mnamo mwaka 2017".

"Ripoti hii inathibitisha tena kuwa safari katika bahari ya Mediterania ni mojawapo ya safari za baharini inayosababisha vifo vingi duniani," amesema Pascale Moreau, mkurugenzi wa ofisi ya UNHCR barani Ulaya, aliyenukuliwa katika taarifa hiyo.

"Kwa kupungua kwa idadi ya watu wanawasili kwenye pwani za Ulaya, swali sio tena ikiwa Ulaya inaweza kusimamia takwimu za wahamiaji wanaowasili lakini badala yake inaweza kuona ikiwa inaweza kutia mble ubinadamu kwa kuokoa maisha ya watu," Bi Pascale ameongeza.