DRC-ICC-SIASA

Chama cha Bemba chatoa wito kwa ICC kuweka mambo sawa

Jean-Pierre Bemba wakati akiwasilisha fomu ya kuwania katika uchaguzi wa Desemba 23 kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi (CENI), katika manispaa ya Gombe, Kinshasa, Agosti 2, 2018.
Jean-Pierre Bemba wakati akiwasilisha fomu ya kuwania katika uchaguzi wa Desemba 23 kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi (CENI), katika manispaa ya Gombe, Kinshasa, Agosti 2, 2018. REUTERS/Kenny Katombe

Chama cha kiongozi wa zamani wa kivita Jean-Pierre Bemba kimetoa wito kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu "kuweka mambo sawa" kuhusu sheria inayomhukumu Bemba kwa kosa la kuhonga mashahidi.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha MLC kinabaini kwamba sababu kuu iliyomuangusha Bw Bemba kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 ni hukumu hiyo ya ICC

Hii ni "tafsiri potofu za sheria ya ICC ili kumzuia Bw Bemba katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23, 2018," katibu mkuu wa chama cha MLC Eve Bazaiba ameandika katika barua iliyowasilishwa kwa Bibi Fabienne Chassagneux, mwakilishi wa ICC nchini DRC.

Mahakama ya Katiba imethibitisha uamuzi wa CENI wa kumzuia kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23na kusema kuwa Jean-Pierre Bemba hana sifa ya kuwania katika uchaguzi huo kufuatia hukumu aliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa kosa la kuhonga mashahidi. Kati ya wagombea sita waliozuiwa na Tume ya Uchaguzi kuwania katika uchaguzi wa urais nchini DRC, wawili wamerudishiwa haki ya kuwania.

Miezi mitatu iliyopita, hakuna mtu aliyefikiria kuwa Jean-Pierre Bemba atakuwa katika kinyang'anyiro cha urais. Lakini kutokana na tangazo la kuachiliwa kwake huru, kiongozi huyo wa zamani wa waasi alikua na matumaini ya kuwania katika uchaguzi wa urais. Alikua hajarudi DRC kwa zaidi ya miaka 10.

Jean-Pierre Bemba anatajwa kama mpinzani mkuu anayesumbua utawala wa Joseph Kabila na chama chake cha PPRD katika uchaguzi ujao.

Hivi karibuni Bemba aliachiliwa katika kesi dhidi ya uhalifu wa kivita na mahakama baada ya kutumikia kifungo cha miaka kumi jela.

Mwezi uliopita alirejea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupokelewa kwa mapokezi makubwa kutoka kwa wafuasi wake