DRC-VYOMBO VYA HABARI-USALAMA

DRC: Mwandishi wa habari aliyetekwa nyara aachiliwa baada ya kutoa fidia

Eneo la Rutshuru linakabiliwa na mdororo wa usalama.
Eneo la Rutshuru linakabiliwa na mdororo wa usalama. GOOGLE Maps

Shirika linalotetea vyombo vya habari limetangaza kwamba mwandishi wa habari aliyetekwa nyara katika mkoa unaokabiliwa na machafuko wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC, ameachiliwa, baada ya siku sita akiwa mikononi mwa watekaji nyara.

Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Tusenge aliachiliwa siku ya Ijumaa Agosti 31, 2018 saa mbili usiku, baada ya familia yake kulipa fidia, "Journaliste en danger (JED) imesema katika taarifa yake.

"Kwa sasa mwandishi wa habari ameruhusiwa kwa matibabu sahihi katika hospitali huko Rutshuru kufuatia mateso ya ukatili aliyopata."

Emmanuel Tusenge Sebazungu ni mkurugenzi wa Radio Umudiho FM, kituo cha Radio kinachotangaza kutoka eneo la Rutshuru (Kivu Kaskazini). Alitekwa nyara siku ya Ijumaa na wapiganaji.

JED imemtaka mwandishi huyo wa habari kufungua mashitaka ya utekaji nyara, kufungwa kinyume cha sheria na kufanyiwa madhila".

Eneo la Rutshuru, kusini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini, limeathiriwa na makundi ya watu wenye silaha kutoka nchi jirani na wanamgambo kwa zaidi ya miaka 20. Visa vya utekaji nyara na kuachiliwa baada ya kulipa fidia vimekithiri katika eneo hilo.