DRC-USALAMA-HAKI

Maafisa wawili wa polisi wakamatwa DRC

Nje ya mahakama ya Goma, wanaharakati vijana walikusanyika wakiwa na mabango ili kuwaunga mkono ndugu zao "Free Lucha," Februari 22, 2016.
Nje ya mahakama ya Goma, wanaharakati vijana walikusanyika wakiwa na mabango ili kuwaunga mkono ndugu zao "Free Lucha," Februari 22, 2016. © RFI/Sonia Roll

Maafisa wawili wa polisi wanaoshutumiwa kuwa hawakuzuia maandamano ya shirika la kiraia la Lucha wanazuiliwa tangu Jumatatu wiki hii huko Kananga, katikati mwa DRC, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.

Matangazo ya kibiashara

Afisa anayehusika na usalama wa ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) na namba 2 wa kitengo maalum cha polisi cha Kananga, mji mkuu wa jimbo la Kasai wanazuiliwa kwa kushindwa kuzuia maandamano.

Wanashutumiwa "kosa la ukiukwaji wa maagizo", "walishindwa kuwajibika" kwa sababu "sio kushindwa tu kuzuia maandamano ya wanaharakati wa Lucha, lakini pia waliacha wanaharakati wa shirika hilo kuingia katika majengo ya Ceni" , chanzo cha mahakama kimeliambia shirika la Habari la AFP.

"Walipelekwa kwenye ofisi ya mwendesha mashitaka ambako wanazuiliwa baada ya kuhojiwa na maafisa wa polisi wa idara ya upelelezi," chanzo cha polisi kimeliambia shirika la Habari la AFP.

Jenerali Fidèle Kawumba, mkuu wa polisi wa Kananga, hakuthibitisha wala kukanusha habari hii: "Hayawahusu ," ameiambia AFP.

Jumatatu huko Kananga, wanaharakati wa Lucha waliandamana hadi makao makuu ya CENI ambapo waliacha waraka ambamo wanataka "kuachana na mashine ya kupigia kura na kutupilia mbali asilimia 16 ya wapiga kura hewa", mwandishi wa AFP ameripotiwa.