DRC-USALAMA

Wawili wauawa katika vita kati ya jeshi la DRC na waasi wa Rwanda

Askari wa DRC (FARDC) wakisihi raia kuwa watulivu huko Miriki, kilomita 110 kaskazini mwa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Januari 7, 2016.
Askari wa DRC (FARDC) wakisihi raia kuwa watulivu huko Miriki, kilomita 110 kaskazini mwa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Januari 7, 2016. © AFP

Watu wawili wameuawa katika mapigano kati ya jeshi la FARDC na waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Watu waliouawa ndio waliuawa katika "mapigano kati ya jeshi letu na waasi wa FDLR", na watatu wamejeruhiwa, msemaji wa jeshi la FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Major Guillaume Djike ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Askari wawili pia walijeruhiwa wakati wa mapigano hayo," ameongezea, akibaini kuwa "operesheni ya jeshi bado inaendelea" katika eneo ambalo linaingiliana na Hifadhi ya Taifa ya Virunga.

"Mapigano yalianza leo asubuhi (JUmatano). Barabara inayotoka Goma kuelekea Rutshuruilifungwa kwa muda. Sisi Tunasikitishwa na vifo vya watu wawili waliouawa kwa risasi hewa, raia wengine watatu walijeruhiwa vibaya," amesema kwa upande wake Eric Mushagiro, kiongozi wa wilaya ya Rugari.

Kundi la waasi la FDLR liliundwa na wakimbizi wa Kihutu wa Rwanda mashariki mwa DRC baada ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda, ambayo yalisababisha vifo vya watu 800,000 kutoka Jmaii ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kundi hili ambalo limeweka kambi yake kubwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, halijawahi kuendesha mashambulizi kababambe ya kijeshi nchini Rwanda tangu mwaka 2001 na mara kwa mara linatuhumiwa kufanya mauaji dhidi ya raia katika maeneo wanayodhibiti.

Eneo la Mashariki mwa Congo limeathirika kwa mapigano na migogoro ya kivita kwa zaidi ya miaka 20, migogoro ambayo inachochewa na migogoro ya kikabila na mizozo ya ardhi, ushindani wa udhibiti wa rasilimali za madini na uhasama katika ya makundi ya waasi.