LIBERIA-UHALIFU-HAKI

Mtuhumiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu nchini Liberia akamatwa Ufaransa

Charles Taylor, kiongozi wa kivita, na Jewell Howard, Gbargna, Julai 26, 1996.
Charles Taylor, kiongozi wa kivita, na Jewell Howard, Gbargna, Julai 26, 1996. © AFP

Mtu anayetuhumiwa kuhusika katika uhalifu dhidi ya binadamu nchini Liberia katika miaka ya 1990, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoikumba nchi hii ya Afrika Magharibi, ameshtakiwa na kufungwa nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Kunti K. raia wa Liberia aliyepewa uraia wa Uholanzi, "alikuwa mmoja wa viongozi katika kundi la ULIMO", kundi lililojumuisha makundi matatu ya waasi yaliyopamdana dhidi ya rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua maelfu ya watu katika nchi hii ya Afrika Magharibi, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.

Kunti K. ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1974 anashtumiwa kuwanyia raia mateso, kuwatumia watoto katika jeshi lake, mauaji na utumwa, kati ya mwaka 1993 na 1997, kama sehemu ya uchunguzi wa mahakama uioanzishwa siku ya Alhamisi na ofisi ya mashitaka ya Paris, kwa mujibu wa chanzo hicho.

Alikamatwa mjini Paris katika eneo la Bobigny, ambapo alikua amejificha kwa rafiki yake, Kanali Eric Emeraux, kamanda wa kikosi kinachopambana na uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji ya halaiki na uhalifu wa vita (OCLCHGCG) ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Aliingia nchini Ufaransa mnamo mwaka 2016, baada ya kuondoka Uholanzi kwa kupitia Ubelgiji," amesema Kanali Emeraux.

Uchunguzi wa awali kuhusu "uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita" ulianzishwa na ofisi ya mashitaka ya Paris kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa Julai 23, 2018 na shirika lisilo la kiserikali la Civitas maxima, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.

Liberia, nchi ya Afrika Magharib ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyogharimu maisha ya watu 250,000 kati ya mwaka 1989 na 2003.