ZIMBABWE-MNANGAGWA-SIASA

Rais Mnangagwa ateua Baraza la Mawaziri

Raisi wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Raisi wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa REUTERS/Philimon Bulawayo

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza Baraza la Mawaziri 20.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kuapishwa kutokana na ushindi wa Uchaguzi wa urais mwezi Julai.

Hili ni Baraza dogo la Mawaziri ambalo limepunguzwa kutoka Mawaziri 30 kama ilivyoshuhudiwa katika serikali iliyopita.

Hakuna wanasiasa wa upinzani walioteuliwa katika Baraza hili.

Aliyekuwa Naibu rais wa Benki ya maendeleo ya Afrika Mthuli Ncube, ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha huku Sibusiso Moyo akiteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya nje.

Wiki hii, rais wa zamani Robert Mugabe, alisema sasa anamtabua rais Mnangagwa kuwa kiongozi rasmi wa nchi hiyo.

Aidha, ametaka wito kwa serikali mpya, kuwaruhusu wapinzani kuandamana kwa amani, kupinga matokeo ya Uchaguzi huo.