MADAGASCAR-SIASA-UCHAGUZI

Rais wa Madagascar ajiuzulu kuwania urais kwa muhula wa pili

Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina  akitangaza kujiuzulu kwake, Septemba 7 2018
Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akitangaza kujiuzulu kwake, Septemba 7 2018 RIJASOLO / AFP

Rais wa Madagascar Hery Rajaona amejiuzulu, ili kuwania urais kwa muhula wa pili.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika tarehe 7 mwezi Novemba.

Katiba ya nchi hiyo, inamtaka rais kuachia madaraka mwezi mmoja kuelekea Uchaguzi mwingine.

Rais huyo sasa anaanza kampeni, akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Didier Ratisraka, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina.

Wapinzani hawa watatu, walifungiwa kuwania urais mwaka 2013 na wanarejea na ahadi za kuimarisha uchumi wa kisiwa hicho na kuunda nafasi za ajira.

Mshindi wa Uchaguzi huu ni lazima apate asilimia 50 ya kura zote, la sivyo kutakuwa na duru ya pili ya zoezi hilo.