SOMALIA-AL SHABAB-UGAIDI

Shambulizi la bomu latikisa jengo la serikali mjini Mogadishu

Bomu limelipuka nje ya Ofisi ya serikali mjini Mogadishu nchini Somalia, na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa na kuharibiwa kwa majengo kadhaa.

Shambulizi la bomu mjini Mogadishu
Shambulizi la bomu mjini Mogadishu REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema, kulisikika mlipuko mkubwa lililolenga ofisi ya serikali katika Wilaya ya Hodan. Vilipuzi vilikuwa vimetengwa ndani ya gari dogo.

“Mlipuko ulikuwa mkubwa sana, hadi sasa hatufahamu idadi ya watu waliojeruhiwa kwa sababu kuna jengo lililoporomoka,” alisema kiongozi wa polisi Ibrahim Mohamed.

Mashambulizi kama haya yamekuwa yakishuhudiwa nchini humo hasa jijini Mogadishu mara kwa mara na kusababisha maafisa ya watu.

Kundi la Al Shabab, limekuwa likitekeleza mashambulizi hasa kulenga ofisi za serikali ya Modagishu.